Habari iliyochapishwa na NPR tarehe 2 juni imefichua kuwa maafisa wa gereza katika jimbo la Michigan nchini Marekani kwa sasa wanapiga marufuku vitabu vya lugha za Kiswahili na Kihispania. Zaidi ya hayo, Kyle Kaminski, Mkuu wa Uhusiano wa Sharia wa Idara ya Marekebisho ya Michigan, alipozungumza na Dkt Anna Belew kutoka Endangered Languages Project (Mradi wa Lugha Zilizo Hatarini), alithibitisha kuwa marufuku hii inaenea kwa lugha zote zisizo za Kiingereza, ikiwa ni pamoja na lugha za asili kama Anishinaabemowin.
Muungano wa Kimataifa wa Haki za Lugha unapinga ukiukwaji huu wa haki za lugha. Tuntetea haki za lugha kwa kila mtu, ikiwa ni pamoja na wafungwa.
Tunawahimiza wanachama wa muungano na wahusika wa umma kuwasiliana na Idara ya Marekebisho ya Michigan, kwa lugha yoyote unayoweza, kueleza hasira yako juu ya ukiukaji huu wa haki za lugha. Maelezo ya mawasiliano ya maafisa husika ni kama ifuatavyo:
Heidi Washington (Mukurugenzi wa Idara): washingtonm6@michigan.gov
Kyle Kaminski (Uhusiano wa Sheria): KaminskiK@michigan.gov
Chris Gautz (Afisa wa Uhusiano wa Umma): GautzC@michigan.gov
Ili kuelewa maelezo ya kesi hii, na kujifunza zaidi juu ya hatua zaidi unazoweza kuchukua, tafadhali angalia viungo vifuatavyo:
Michigan Abolition and Prisoner Solidarity phone zap: tinyurl.com/2p8nn7st
Kommentare